-->

Feisal salumu zangumza

0


🚨#Repost absam

Kwa ridhaa ya Wananchi, Mabingwa wa muda wote naombeni kuongelea kwa mara ya mwisho sakata la mdogo wetu na kilichotokea jana;

Mwanetu kwa mara nyingine tena aliandika barua ya kutaka kuvunja mkataba akaipeleka TFF akiwataka wajunje mkataba.

Tulivoitwa mbele ya chombo cha TFF chenye hadhi ya kimahakama (Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji) Yanga tuliweka mapingamizi manne;

1. Tunaamini Kamati imeshasikiliza na kutoa maamuzi ya suala hili linalohusu uvunjifu wa mkataba “Contract termination“ kwenye maamuzi ya kwanza na ya review, hivo shauri hili la leo ni “res judicata”.

2. Kwakuwa suala hili limeshasikilizwa na kutolewa maamuzi hapo awali, hivo mikono ya kamati imeshafungwa na sheria“functus officio”.

3. Kwa kuwa mikono ya kamati imeshafungwa na sheria kusikiliza tena hili suala, kamati haina tena mamlaka ya kusikiliza hili suala “Jurisdiction”.

4. Pia mkataba unaotaka kuvunjwa wahusika ni Yanga na Fei, ndio wanauwezo wa kuvunja mkataba TFF sio wahusika wa mkataba huo hivo hawana uwezo wa kisheria kuvunja mkataba wakati wahusika hawajakaa kutaka kuvunja mkataba na kushindwana “Privy to contract”.

Hoja hujibiwa kwa hoja, mambo ya sijui mimi namuwakilisha Drogba, sijui nani hayatuhusu, hata kama ungekuwa unamuwakilisha Messi na Ronaldo, dakika 10 ni nyingi sana kujibu hoja.

Mwisho; Fei ni ndugu yetu, anakaribishwa muda wowote kuja Yanga kuleta maombi ya kuvunja mkataba na atapewa baraka zote na huu ndio msimamo rasmi wa Yanga.

Ndugu zangu waandishi wa habari, saidieni mpira wetu kwa kutoa elimu na taarifa sahihi, si kukata vipande vya video kwa lengo la kutengeneza content, mna mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya soka la Tanzania na jamii inawategemea sana.

Jumaa Mubarak 🙏🏿
@yangasc @yangasc @yangasc 

#twenzetukwamadiba 
#daimambelenyumamwiko🔥🔥💚💛



 

Tags

Post a Comment

0Comments

123

Post a Comment (0)