KCB Bank Tanzania yaandaa mahafali ya wanufaika 295 2jiajiri mkoani Mwanza!
Benki ya KCB imeandaa mahafali ya vijana 295 chini ya mpango wa KCB 2jiajiri mkoani Mwanza.
Hii ni sehemu ya ushirikiano wa Sh2.2 bilioni kati ya KCB Bank Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ili kuwawezesha vijana 960 katika sekta ya ujenzi.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mh.Hassan Massala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ambaye aliipongeza Benki ya KCB kwa jitihada zake za kuwawezesha vijana nchini Tanzania na kusisitiza kuwa itasaidia kuboresha maisha sambamba na kujenga Taifa linalojitegemea kwa kuboresha nguvu kazi ya nchi na kupunguza changamoto ya ajira.
Mbali kutoa huduma za kifedha, KCB Bank ina dhamira ya kubadilisha maisha kwa kufungua milango mbalimbali ya fursa na tuna furaha kwa kutekeleza mradi huu kwa ufanisi huku tukiamini utakuwa ni mradi wenye matokeo chanya na ya kudumu katika jamii.
#kcbbanktz #ForPeopleForBetter
123