-->

Habari

0

KATAVI: Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Amos Makalla amesema “Asije Mwanasiasa akakudanganya kuwa anao uwezo wa kubadili maamuzi ya Mahakama, tunaamini chombo cha kutoa haki kikatiba ni Mahakama. Tupo tayari kusikiliza kero zozote ambazo hazijaingia kwenye Mhimili wa Mahakama ili kupata haki"

Ameongeza “Lazima Watu wetu wajue mambo yaliyo Mahakamani yanamalizwa Mahakamani, tutakachokupa ushauri ni kukata rufaa. Ukweli lazima usemwe itakuwa tunawadanganya tu Watu kwamba hili unajua lipo Mahakamani tutakusaidia, sio kweli.”

Naye, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema “Hatutagusa masuala ambayo yapo Mahakamani, ndio utaratibu wa Utawala Bora, moja ya Sera muhimu ya CCM ni kusimamia Utawala wa Sheria. Wakati wote tutakuwa tunahamasisha na kuziwezesha Mahakama kutenda haki bila kuingiliwa katika maamuzi yake.”

Tags

Post a Comment

0Comments

123

Post a Comment (0)