Tafakuri
Salam kwa MAMA kuelekea MEI MOSI
MAMA yangu hatujatenganishwa na ukuta hivyo pokea Salam zangu, Ni mimi mwanao JAZA UONE leo nimeamua nikusalimie tu
MAMA yangu wakati wafanyakazi wakienda kusherekea sikukuu yao ya wafanya kazi MEI MOSI Leo naomba nikukumbushe kidogo,
MAMA yangu pamoja na yote uliyowaza kuyafanya siku ya MEI MOSI nikuombe uangalia Sana swala la nyongeza ya MISHAHARA kwa watumishi wa UMMA,
Binafsi nitaongelea sekta chache za watumishi wa umma hasa tunaoishinao uku mitaani,
MAMA yangu kama ikikupendeza jicho lako litazame Sana sekta ya ELIMU, KILIMO, AFIYA, UVUVI , WATENDAJI wa vijiji, WATENDAJI wa KATA, nk,
MAMA yangu nimezitaja sekta hizi chache kwani hawa walio wengi tunaishinao uku vijijini, ukweli wanaishi maisha magumu sana kutokana na GHARAMA ZA MAISHA KUWA JUU uku mishahara yao ikiwa midogo, hivyo kupelekea kuishi maisha ya kuunga unga, uku wakikosa hata bando la internet la siku,
MAMA yangu nakukumbusha tu hili mapema ikikupendeza liweke kwenye HOTUBA YAKO YA MEI MOSI, kama kuna sehemu jicho lako linatakiwa litazame Sana basi Ni hizo sekta, HASA NYONGEZA YA MISHAHARA
MAMA yangu wakati nikiendelea kukusisitizia juu ya kupandisha MISHAHARA hasa kwenye hizo sekta basi ningependa kukuomba kwenye hotuba yako ibebe tumaini jipya la ndugu zetu walioitimu VYUO na bado wanasubiri AJIRA, na pia kwa watumishi sekta ambazo kwa mda mrefu hawajapandishwa maraja kazini,
MAMA yangu yangu umefanya Mambo mengi sana kwenye sekta ya ELIMU ,umejenga madarasa mengi na kuanzisha shule mpya ,ila nikukumbushe tu
MAMA yangu hata hayo madarasa ya mwanzo WAALIMU walikuwa WACHACHE tena adi mzee alipowaondoa watumishi hewa ndo alizidi kuwapunguza kabisa,
MAMA yangu hatuna shida ya waalimu kusema tukachukuwe nje ya NCHI kwani wahitimu wapo wengi mitaani wanasubiri AJIRA,
Madarasa bila waalimu bado hatujamkomboa mwanafunzi, HAPA MAMA PAANGALIE KWA JICHO LA PILI,
MAMA yangu kwenye sekta ya afiya nako umewekeza Sana tunaona zahanati na vituo vya afiya vinavyo jengwa kila sehemu, bado changamoto ni watumishi hawatoshi kabisa, kwani Sasa hivi unaweza kwenda KITUO CHA AFIYA au ZAHANATI ukawakuta WATUMISHI wawili au mmoja, wakati huo kituo au zahanati hiyo inaudumu zaidi ya vijiji Vitatu au vinne, HAPA MAMA PAANGALIE KWA JICHO LA PILI,
MAMA sekta ya KILIMO imebeba sehemu kubwa ya MAISHA YA WATU, pamoja na MAAFISA KILIMO tulio nao ila kwa uchache wao uku vijijini tunalima kilimo cha kubahatisha tu, hivyo na HAPA MAMA PAANGALIE KWA JICHO LA PILI,
MAMA yangu siku zote nilikuwa najiuliza kwa nini sasa hivi RUSHWA imeamia kwenye sehemu za KUITAFUTA HAKI, hapa napo nikagundua Ni MISHAHARA MIDOGO waipatayo wasimamizi wa haki ndo inapelekea RUSHWA acheze sana maeneo hayo, hivyo HAPA NAPO PAANGALIE KWA JICHO LA PILI,
Mama nina mengi ya kukuomba uyaangalie ,ila kwa leo niishie hapa ,niendelee kukusisitizia juu ongezeko la MISHAHARA na AJIRA , HILI NI MUHIMU KULIKO POSHO ZA WABUNGE NA MAWAZIRI
Pokea Salam zangu
Bado
naendelea kusoma nje ya darasa
123