Baada ya kimya cha muda mrefu, mwanamuziki Profesa Jay amepost picha yake hiyo na kueleza yafuatayo
"Salaam ndugu zangu, Kwanza namshukuru sana Mungu aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, hali yangu ilikuwa mbaya isiyoelezeka, asante sana Mungu Baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu).
Pili, kipekee namshukuru sana Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mama yetu Dr. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na nje ya Nchi, Asante sana mama pamoja na Serikali yako yote kwani viongozi wako wa chama na Serikali walikuwa wanapishana kuja kuniona na kunifariji.
Tatu namshukuru sana Mwenyekiti wa chama changu cha CHADEMA Kamanda Freeman Mbowe , wanachama na viongozi wote waandamizi wa chama kwa jitihada zao za kuhakikisha napata matibabu bora zaidi kwa kushirikiana na Serikali, zaidi nawashukuru sana Madaktari na manesi wote wa Muhimbili na kote nilikopitia kwa kunipa matibabu ya kiwango cha juu kwa zaidi ya mwaka mzima niliolala hapo Muhimbili hasa zile siku 127 za hatari nilizokuwa nimelazwa ICU, mlijitoa kwa uwezo wenu wote kuhakikisha kuwa mnaokoa uhai wangu, ASANTENI SANA
Mwisho na kwa umuhimu mkubwa sana nawashukuru sana Watanzania wote mliojitolea kwa maombi na michango ya fedha zenu kuhakikisha natibiwa na kusema ukweli ilinisaidia sana kulipa bills za awali kabla ya Serikali kuamua kuingilia kati na kuubeba mzigo huu, asanteni sana na sitowasahau"- Ameandika Profesor Jay kwa mara ya kwanza tangu aliporipotiwa kuugua kwa zaidi ya mwaka na miezi kadhaa"
123