UMRA bint kijakazi_____34__35
MTUNZI Malkia
safari yangu ya kwanza nilienda mpaka kule Kijijin kwa mganga wa kienyeji ambapo niliwahi Kumuona baba akimpeleka crack
"Habari za sahizi" nilisalimia Baadhi ya wakina mama Walio Kuwa pale
Salama tu karibu
"Ahsante Huduma ipo Kweli" niliuliza pale Nje
"Huduma Anatoa ila foleni ndo kama unavyoona "
"Mmh" niliguna Baada ya Kuona Watu ni Wengi mno
Tukiwa hapo niliamua kutulia kama nitapata Nafasi ya Kuingia ndani licha ya Kufika hapo Sikua Hata najua kama nitapata Nafasi ya Kumuona huyo mtaalamu nitaongea nae nini ??
Alipota Mkaka Mmoja akiwa Smart sana
"Hee Kaja na leo mika Huyoo" nilisikia wale wamama wanaongea huku wanaoneshana nilipp geuka nilimuona Huyo kaka waliomtaja kwa Jina la mika
"Ila mikoo mingine jamani mmh Mkaka Mzuri Kumpa mauganga ndio nini afu anahela na elimu yake Uyo " nilimtazama yule Mkaka ambae Alikua anakuja njia ya Upande Wetu
"Hee Umra mi wewe eeh" Nilishangaa ananitaja Jina langu nilipo Mtazama sura yake kwa mbalii Ilikua kama naijua Lakini sikufaham niliwahi Kumuona wapi
"Ndio mamboo" nilimjibu huku naendelea kutathimini kama nitakumbuka wapi nilimuona
"Vipi ulikua unahitaji huduma kwa mzee"
"Ndio " wakati najibu nilikua nawatizama wale wa mama sura zao wazi walijuta kwa Walio Kuwa wanaongea mbele yangu
"niliinuka nikaongozana nae tulienda Mpka Kwenye kile kijumba ambacho ile Siku kuna Mkaka alinisaidia na kuniingiza humo
.
"Nilipoona Picha Yako nilifikiri nimekufananisha Kumbe Kweli ni wewe" sikumuelewa hata Ilibidi niitike tu
"Abeee"
"Hunikumbuki kwani???"
"Naomba unikumbushe"
"Mmh umraaa!! Umesahau uliewahi kuingia humu ndani na ulikuja kwa Ajili ya kumtafuta Ndugu yako"
"Oooh Nimekumbuka yule kaka Yupo wapi alinisaidia sana ile Siku"
"Hahah Umra ni mimi Bwana kwahy Humjui Hata aliekusaidia ile Siku"
Mmmh Nilishtuka Kidogo Yaan Kweli sura Inakuja Ila Muonekano ni Tofaut kabisa
"Ni mimi Bwana ile siku labda Ulikua na Haraka Haraka enhee leo tena nini kimekuleta?? Naona leo umefata Utaratibu Kuliko Kufata fata kuta zingine Zisizo Kuhusu"
"umejuaje jina langu"
"Hahaha umraaaaaa!!" Alicheka Huku anainuka Kuingia Kwenye Moja ya Chumba kilicho Kweny Hiyo Nyumba bila hata kunijibu Baada ya Muda Alitoka akiwa na mavazi kama yale ya Siku ile SÃ sa Hapo ndo Picha kamili ilikuja maana Alionekana kama mganga au msaidizi wa mganga
"Mhuuu haya niambie Shida nini Bint"
alikua ananiuliza huku anakaa chini alipo tandika shuka Nyekundu Chini
"umejuaje jina langu ile Siku wala sikukutajia Jina"
Nilihisi Huenda Inaweza Kuwa ni mtego Tayar wameshanijua hawa
alitoa simu yake Kubwaa na Inaonesha ni ya Gharama sanaa akaibonyeza kwa sec kisha akanipatia mbele Kulikua na Picha yangu hata Sijui imefika Vipi sikumbuki hata mara ya Mwisho Mimi Kupiga Picha Sijui ile picha ilipigwa Vipi na lini Sikuwahi Hata kuiona
"mimi Naitwa mika hapo Kati nilikua Natafuta mchumba na mdogo wangu ndo alinipatia hii picha yako nilihisi hii sura naijua Kabisa lakini Sikua na Uhakika Mpaka leo nilivyokuona "
Nilishindwa kabisa Kuficha Mshangao wangu kumbe Huyu ndo Mchumba niliekuwa nawasiliaba nae Yaan mganga wa kienyeji Uuuh Mapya haya sindo Kule Kule kwa kina kagome Tena narudishwa miee Nilikua Kimyaa kichwan mawazo ya kila Rangi yalipita
"ulivyonambia nilikuelewa hata usijali Umra"
"aaah Asantee kwa kunielewa"
"najua kuna mtu ameujaza moyo wako Sijui ni nani hata Hivyo Hongera nikupe tu,,,ouky unaweza kuniambia shida yako au ni lazima uonane na mzee"
nilikua nikimtazama tu huku namtathimni nimuweke kundi Gani Mkaka kijana na smart kabisa afu anakua mganga mmh
nilijishtukia baada ya kuona ananitazama Sana
"aah mmh hapana wewe unaweza kunisaidia Zaidi Maana imekua kama hatma Kuendelea kukutana mimi nawewe tunaweza kuongea kama Marafiki??"
"Ooh nimependa hiyo Umra mhuu niambie SÃ sa Mimi nitakua Zaidi ya Rafiki kwako"
"kuna mtu wanguu wa Karibu Sana amekua Mwehu na kupotea kabisa hajulikani alipo"
"ni nani Jina lake nami unataka Nikusaidie aje Umra Kuwa Huru wala usisite kama kipo ndani ya uwezo wangu nitakusaidia"
Sikujua nianzie wapi niseme Ukweli au nidanganye niliingiwa na Woga sana
"Umra hauniamin bado ?? Au unaniogopa??"
"Hapana"
"Hapana Ukiwa na Maana"
"wala sikuogopi"
"Hayaa nakusikia "
"ndo hivyo tu amekuwa mwehu na simpati hata Naomba unisaidie nimpate nakuomba Tafadhali apone Kabisa"
Wakati huo nilipiga Kabisa magoti mbele yake na Machozi Juu
"ah aaah!! Inuka Inuka Umra usifanye Hivyo bwana Inuka " aliniinua na kunikalisha tenaa
"Umra anaombwa Mungu tu sio Binadamu Kipenz Sawa eeh mimi kama matatizo yake yanahusiana na Binadam nitakusaidia ila kama ni uwezo wa mungu hapana ilo tutamwachia Yeye tu....jina lake nani??"
"Anaitwa crack "
"Jina la mama Yake"
"Yusra"
"Oukay"
Alitulia Akiwa anafanya fanya Vitu hata Sivielewi kabisa
akiwa ameshika chungu alishtuka Mpak kikaanguka chini
Itaendelea.....
UMRA bint kijaKazi______35
MTUNZI Malkia Osam
Wasp 0710066699
alishtuka kisha akanitazama kwa Dakika Mbili nzimaa Moyo wangu ulikua Unaenda Mbio sana Sikujua uso wake ni wa shali au vipi
"Ni nani yako huyu"
"Ni..ni Huyu ni ndu..ni ndugu yaa..ngu" nilikua naogopa Kusema ukweli lakini nilisita kudanganya
"Umraa huyu mtu huyuu duuh mimi Uwezo wa kumsaidia sina"
niliogopa majibu yake nilihisi kukataa tamaa kabisa mpaka chozi lilinitoka
"Umra sikia huyu Mtu anaagano na jini Yeye amefungishwa ndoa na jini kuu ,,,Yeye kakosea mashart kaenda kutembea na Mwanamke Mwingine kwahiyo anatumikia adhabu yake kibaya Zaidi Mwanamke huyu ni Mjamzito bora hata angekuwa hana mimba angesamehewa"
niliishiwa nguvu kabisa mwili wote uliregea kwa Taarifa Hizo nilijiona nimekata tamaa kabisa
"sà sa natakiwa kufanya nini Ili nisaidie mimi nataka kumsaidia"
"Unamjua huyu Mwanamke Mwenye ujauzito wake"
"Ndio nina mjua"
"sà sa huyu Mwanamke apatikane ukubali Kutoa Sadaka Hicho Kiumbe Ili yule afunguliwe ila atabaki Kuwa Tahira Hawezi Kupona kabisa kwa hapa ninachoona alikua Tahira hizi ndoa hizi lazima upungue akili"
"Ni Bora awe Tahira Lakin apatikane Sijui hata alipo huyo Mwanamke"
"Nitajie Majina yake"
"namjua tu kwa Jina la Rose"
"Okay"
alitulia kwa sec kadhaa Baada ya Mimi kutaja Jina mwanamke ambae nina Uhakika Aliondoka na mimba ya crack Wangu
"Umraa" aliniita Baada ya Kumaliza Vitu alikua anafanya
"abee"
"Huyu rose Huyu hana ujauzito Wowote wala Hajawah kuunganisha Damu na Crack Yaan hawajawahi kuwa na uhusiano wa Kimapenzi ila Inaonekana walikua tu karibu,,, mwingine nani Lbda tumtazame"
Moyo wangu ulishtuka Haswaa Nilianza Kupiga hesabu za haraka haraka nani anaweza kuwa mwingine nanii sikupata hata wa kumuhisi
Niliomba aniambie hata alipo tu akanambia hawezi jua mkoa alipo Lakini Inaonekana yupo magharibi ya tulipo sie Yaan mikoa inayopatikana Upande wa magharibi ,tuliongea mengii sana siku hiyo hata nilijikuta ninamzoea kabisa na kuwa huru
Nilimuuliza Kwanini Yeye anaonaekana anasura mbili
Akanambia ni babu yake tu na mizimu zake zinamsumbua Et awe mganga amejitahidi sana kuikwepa Lakini Kilà akifanya Hivyo Anajikuta Anapata matatizo sana Kazini hivyo Lazima Aje tu kwa babu yake hapo ,nilimuuliza kazi gani anafanya akasema Yeye ni Doctor huko Mjini hospital Moja Kubwa tu alionitajia
Alimbia Umra Mimi siyapendi haya mambo hata Kidogo lakini babu amenichagua mimi bado natafuta Njia ya kuondokana na hili na nitaipata tu japo nashkuru mungu ninasaidia sana Watu
Mwisho tuliondoka Huku akinipa Lift Mpaka Nyumban
Akili yangu iliniambia Nianze zoezi la kumtafuta crack Kwenye Hiyo mikoa Kulikua na mkoa Mmoja tu Upande Wetu wa magharibi kila ni Mpaka wa Kuingia Nch jirani Hivyo Haikua Ngumu mimi kuwaza ni mkoa upi
asubuh nilimuaga wifi nikamuacha anitazamie dukani kwangu safari Ilianza Kuelekea mkoa wa kigoma ambapo Nilihisi Anaweza Kuwa Uko
Nilifika kigoma majira ya Jioni kabisa pale pale stand Nilianza Kutembea Huku nikionesha Picha ya Crack nilizunguka mpaka usiku unazidi nilikua nimechoka sana nikachukua Chumba lodge nipumzike
Asubuh niliendelea na zoezi Baada ya Kupata Chochote kitu nilizunguka na kuzunguka kona zote Lakin sikumpata wala Dalili zozote zile hata Kwamba alikuwepo nilikaa wiki zima nilianza kushikwa na homa za Hapa na Pale nilianza kuamini itakuwa mika ni muongo hata nilijuta Kuamini Maneno yake na kuamua kufata japo moyoni Nilitaman iwe kweli nimuone Tena crack wangu nilikua natembea Huku machozi yanatoka tu
Mwisho nilikata tamaa Baada ya Kuona jitihada Zangu ni bure hazina matunda yeyote ,,,muda huo nilikua kwenye gari nimechoka sana siku hata na Ham ya kuishi kabisa nilijikuta najiona mimi ni mtu wa Mkosi sana tangu kuzaliwa kwangu Maisha yangu Sikuwahi kuyafurahia Kabisa nilikua nakumbuka Vipindi Vyote tangu nilipo kuwa na crack kuna muda nilitabasam nilipo Kumbuka tulipo Anzia na kufika mbali Kiasi hiki Mhu Mungu kweli wa ajabu, ajabu sana Yaan nimeolewa kwa Miaka mitatu nineishi na Mume wangu afu nakuja kutolewa Usichana wangu na Mtu Mwingine Kabisa ,Kwahy Crack ndie mwanaume niliemchagua licha ya mapungufu yake nilimkumbuka mke Mkubwa nilimshukuru sana Maana Yeye Ndio kanipa Maisha haya ya pili
nilikumbuka kuwa crack anandoa na Jini et mimi ndo Sababu na huyo mwenye mimba ya Crack ni nani Kichwa kilimuuma Sana nikachukua Dawa kwenye mkoba wangu Ili ninywe nikagundua sina maji ya kunywa kama Dakika Mbili gari ilisimama kupakia abiria na kushusha niliona ngoja ninunue maji hapo nikachungulia dirishani Ili niite muuza maji Mungu wangu Nilihisi nimelala kwenye siti huenda naota
Nilipiga kelelee kwa Nguvu mnooo
123